JKCI, HOSPITALI YA RUFAA CHATO KUTIBU MOYO KISASA

 

JKCI, HOSPITALI YA RUFAA CHATO KUTIBU MOYO KISASA

JKCI, HOSPITALI YA RUFAA CHATO KUTIBU MOYO KISASA

TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato imeanza kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa kutumia mashine za kisasa ambazo zina uwezo wa kugundua magonjwa ya moyo kwa usahihi wa asilimia 95.
Huduma hizi zinatolewa wakati wa maonesho ya 7 ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili, mjini Geita ambapo huduma hizo zinafanyika katika mikoa ya pembezoni mwa Tanzania ili kuwasogezea wananchi huduma za kibingwa.
Tanzania ni nchi peke iliyopewa jukumu la kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na inahakikisha inafikia wananchi wengi zaidi, hususan wale walioko mikoani.
Ushirikiano kati ya JKCI na CZRRH ulianza mwaka 2022 kwa lengo la kuikuza hospitali hiyo na kuiwezesha kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo kwa ufanisi zaidi.
Kupitia ushirikiano huo, hospitali hiyo imeanza kutoa huduma za upasuaji wa mishipa ya damu na hadi sasa wagonjwa wanne wamefanyiwa upasuaji huo kwa mafanikio.