TMA YAKABIDHIWA RADA MBILI

 

TMA YAKABIDHIWA RADA MBILI

TMA YAKABIDHIWA RADA MBILI

DAR ES  SALAAM
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekabidhiwa rasmi rada zake mbili za hali ya hewa zilizopo Mwanza na Dar es salaam zilizokuwa zinafanyiwa uboreshaji na kampuni ya Enterprises Electronic Corporation (EEC) kutoka Alabama, Marekani (USA).
Maboresho hayo  yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia bajeti ya maendeleo yaliyolenga kuboresha (upgrading) ufanisi wa rada hizo zilizokwisha tumika kwa zaidi ya miaka 10 kwa kutoa vifaa vyenye teknolojia yenye software ya kizamani (edge 5) na kufunga ya kisasa (edge 6) ili kupata picha nzuri itakayoweza kutafsiriwa kiurahisi.
Maboresho hayo ni muhimu kwani yatawezesha kuendana na teknolojia inayotumika katika rada nyingine za hali ya hewa zilizofungwa hivi karibuni katika mikoa ya Mtwara, Mbeya na Kigoma na hivyo kutumika katika mfumo jumuishi wa rada (MOZAIC)
 FAHAMU:-  Serikali  imeendelea na  uboreshaji wa miundombinu ya hali ya hewa ikiwemo ununuaji na ufungwaji wa rada tatu za hali ya hewa katika mikoa ya Mtwara, Kigoma na Mbeya na kufanya kuwa na jumla ya rada tano mpaka sasa ikiwa ni matazamio ya kufikia mtandao wa rada saba hapa nchini.
 RADA HIZI ZINAUWEZO WA KUFUATILIA MATUKIO YA HALI YA HEWA KWA UMBALI WA NUSU KIPENYO CHA ZAIDI YA KILOMITA 250.