TANZANIA KINARA UMILIKI WA RADA AFRIKA MASHARIKI, KATI

TANZANIA KINARA UMILIKI WA RADA AFRIKA MASHARIKI, KATI

TANZANIA KINARA UMILIKI WA RADA AFRIKA MASHARIKI, KATI

Tanzania inatazamiwa kuwa na rada saba mwishoni mwa mwaka huu na kuifanya kuwa nchi yenye idadi kubwa ya vifaa hivyo kati ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.
Maendeleo hayo yanatokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu ya kisasa ili kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa taarifa za hali ya hewa.