MAKAMPUNI YA KOREA KUWEKEZA TANZANIA
DAR ES SALAAM
ZAIDI ya makampuni 38 ya Korea na 50 ya hapa nchini Tanzania yameonesha nia ya kufanya uwekezaji wa ubia kwenye sekta za maji, miundombinu, mafuta, gesi na madini nchini Tanzania.(Hii ni kwa mujibu wa semina ya miradi iliyofanyika jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha wawekezaji kutoka Korea na Tanzania).
Hatua hizo zimefikiwa baada ya Mhe Rais Dkt Samia kufanya ziara nchini Korea mwezi juni mwaka huu 2024 ambapo aliibua fursa za kiuchumi za Tanzania katika maeneo mbalimbali.
SOMA PIA https://x.com/Bimkubwatz/status/1850791227794379117
Semina hiyo iliratibiwa kwa pamoja na kituo cha uwekezaji (TIC), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Wakala wa Kukuza Uwekezaji wa Biashara wa Korea (KTIPA).
Aidha ushirikiano wa uwekezaji kati ya makampuni ya Tanzania na Korea uko tayari kuwezesha teknolojia baina ya raia wa nchi hizo mbili sambamba na kubadilisha ushirikiano baina ya nchi hizo kuwa wa kilele kipya.
Balozi wa Korea nchini, Ahn Eunju, amesema ziara ya Mhe Rais Samia nchini Korea ilizifanya nchi hizo mbili kukubaliana kuanzisha mazungumzo ya Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi ambao ni wa kwanza kwa nchi hiyo ya Asia kuanza na Tanzania.
Amebainisha kuwa kutokana na ziara hiyo, nchi hizo mbili zilitia saini Mikataba miwili ya Makubaliano (MoUs) kuhusu uchumi wa bluu na maendeleo muhimu ya madini, ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi miongoni mwao.
#ZIARAZABIMKUBWAZINALIPA
