DKT SAMIA KUHUDHURIA MJADALA WA KIMATAIFA WA NORMAN NCHINI MAREKANI
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo Oktoba 29, 2024 kuelekea De Moines Lowa nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria mjadala wa kimataifa wa Norman E.Borloug ulioandaliwa na Taasisi ya world food prize Foundation ya nchini humo.
Mhe.Rais Dkt Samia ni miongoni mwa maRais wanne kutoka Afrika (Tanzania,Sierra Leone,Madagascar na Nigeria) waliopewa heshima ya kushiriki na kuchangia mjadala huo wenye kaulimbiu isemayo “Mbegu za fursa kuunganisha vizazi na kustawisha diplomasia ( seeds of opportunity bridging generation and cultivating Diplomacy)
Mjadala wa kimataifa wa Norman E.Borloug hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na viongozi, wataalamu na watu mashuhuri, watunga sera husussan za kilimo ,lishe na usimamizi wa rasilimali ambapo lengo la majadiliano hayo ni kutafuta suluhu ya changamoto ya upatikanaji wa chakula duniani ambayo inachiochewa na mabadiliko ya tabianchi.
Pamoja na mjadala huo Mhe Samia atashiriki utoaji wa tuzo ya food prize kwa mwaka 2024 kwa watu wenye mchango mkubwa kwenye sekta ya kilimo ikiwa ni muendeleo wa kumuenzi Hayati Dkt. Norman E.Borloug aliyehamasisha usalama wa chakula kwa watu wote duniani.
Vilevile Mhe Rais Dkt Samia atakutana na kufanya mazungumzo ( Round table discussion) na viongozi kutoka serikali na sekta binafsi ya Marekani hususan waliopo kwenye sekta ya kilimo kwa lengo la kujadili uwekezaji katika sekta hiyo na kuongeza Mnyonyoro wa thamani katika sekta ya kilimo ambayo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.
#BiMkubwaTanzania
