SERIKALI KUFUFUA RELI, BANDARI NCHI ZA SADC
ARUSHA
Serikali iko mbioni kufufua reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kuimarisha usafiri wa reli unaounganisha Bandari ya Dar es Salaam na nchi za Kusini mwa Afrika hususan zile za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).Hii ni kwa mujibu wa kikao cha 17 cha mkutano wa mapitio ya utendaji kazi cha uchukuzi kwa mwaka 2024 cha wizara ya uchukuzi kilichoafnyaika Mkoani Arusha.
Kufufuliwa kwa reli ya TAZARA ni hatua muhimu kwa uchumi wa nchi zote zinazotumia reli hiyo kwani awali reli hiyo ilibuniwa kubeba mizigo yenye uzito wa tani milioni 5.5 kwa mwaka, lakini haijawahi kufikia lengo hilo ambapo mwaka 1986, TAZARA iliweza kusafirisha tani milioni 1.2, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kilichowahi kufikiwa.
Reli ya TAZARA ilianza kujengwa mwaka 1970 na kukamilika mwaka 1975, ikiwa na urefu wa kilomita 1,860 na ilijengwa kwa mfumo wa Cape Gauge, tofauti na reli nyingi ambazo zimejengwa kwa mfumo wa Meter Gauge na Standard Gauge hivyo umaalumu wa reli hiyo unalenga kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na nchi jirani.
