TSH MIL 597.6 ZAWAPATIA MAJI KILEWANI
RUKWA
Serikali imepeleka kiasi cha shilingi 597.6 kwa ajili ya mradi wa maji uliotekelezwa katika kijiji cha Kilewani Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa.
Mradi huo ni miongoni mwa miradi iliyojengwa kwa fedha za Mfuko wa Taifa wa Maji (National Water Fund) na unahudumia wakazi wapatao 3,847.
