MRADI WA MAJI NYAKANAZI KUNUFAISHA WANANCHI 4500
KAGERA
Jumla ya wananchi 4500 wa kijiji cha Kasato kata ya Nyakanazi Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wameondokana na shida ya upatikanaji wa maji baada ya mradi wa usambazaji maji chini ya Wakala wa Usambazaji wa Maji Vijijini – Ruwasa kukamilika mradi ambao umetumia kiasi cha shilingi milioni 316.
Mradi wa maji Kasato umehusisha ujenzi wa tenki lenye ujazo wa Lita 50,000 na umejengwa ndani ya miezi sita na umekamilika kwa 100%.
