ZAHANATI YA KIONGERA KUPANDISHWA HADHI
MARA
Serikali imepanga kuipandisha hadhi Zahanati ya Kiongera iliyopo katika kata ya Susuni Halmashauri ya wilaya Tarime Mkoani Mara kuwa kituo cha afya ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024 imepeleka fedha shilingi Milioni 207 kwenye Zahanati hiyo kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Wazazi lenye huduma ya upasuaji wa dharura na jengo la Maabara.