LESENI 6 USAFISHAJI MADINI ZATOLEWA

LESENI 6 USAFISHAJI MADINI ZATOLEWA

 LESENI 6 USAFISHAJI MADINI ZATOLEWA

DODOMA
Serikali imetoa  leseni kwa viwanda sita (6)  za usafishaji madini  ambapo jumla ya dhahabu yenye uzito wa gramu laki 6 na thamani ya shilingi bilioni 84.43 zilipelekwa kusafishwa katika viwanda hivyo vilivyopewa leseni.
Aidha Serikali imeendelea kuvutia uwekezaji katika viwanda vya kusafisha dhahabu kwa kupunguza tozo ya mrabaha kwa madini hususan dhahabu inayopelekwa katika uchenjuaji kutoka asilimia 6 hadi asilimia 4.
Lengo ni kuhakikisha viwanda vya kusafisha madini vinapata malighafi ya kutosha katika kipindi chote.