WANAOKWENDA NJE KWA MATIBABU NI 3% TU
KILIMANJARO
Kutokana na uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya miundombinu, vifaa na vifaa tiba imefanikisha kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopewa rufaa ya kwenda nje kwa 97% huku 3% pekee wakienda kutibiwa nje ya nchi.(Hii ni kwa mujibu wa wizara ya afya wakati wa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na viogozi wa kata 170 katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali, 2024 Mkoani Kilimanjaro).
Hatua hii imefikiwa baada ya jitihada za serikali ya awamu ya sita kuwekeza teknolojia ya kisasa katika Hospitali zote nchini ikiwa ni kutekeleza uboreshaji wa huduma za afya kwa jamii ili kila mwananchi apate huduma bora za afya.