TSH BIL 561 KUONGEZA NGUVU MSD
DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Afya imepokea maelekezo ya kamati ya kudumu ya Afya na masuala ya UKIMWI waliyoyatoa ya kuitaka wizara ya afya kuendelea kuisimamia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa kuipatia mtaji wa Bilioni 561.5 ili kuongeza nguvu kwenye uzalishaji na uendelezaji wa viwanda vya dawa, vifaa na vifaa tiba ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa hizo kwa wananchi, hatua ambayo itaimarisha zaidi upatikanaji wa huduma bora za afya nchini.