MIRADI YA MAJI 1,342 KUTEKELEZWA BAJETI 2024/25
TANZANIA
Serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 imepanga kutekeleza miradi ya maji 1,342 (1,095 vijijini na 247 mijini) katika maeneo mbalimbali nchini.
Serikali inatekeleza Miradi hiyo ili kufikia malengo ya ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 inayoitaka serikai kufikisha huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 85 vijijini na 95 mijini ifikapo mwaka 2025/26.