WANANCHI 6,630 WAPATIWA HUDUMA YA ULTRA SOUND,X-RAY
SONGWE
Wananchi wapatao 4870 wamepatiwa huduma za Ultrasound ikiwemo wajawazito huku wengine wapatao 1760 wakipatiwa huduma za Mionzi(X-Ray) katika Hospitali ya Wilaya ya Songwe ikiwa ni miaka mitatu tangu kuanza rasmi kutoa huduma hiyo katika Hospitali hiyo hali iliyopunguza rufaa kwa wagonjwa.
Serikali imepeleka Mashine za UltraSound za kisasa na zinazotoa huduma kwa wajawazito na huduma zingine zinazohitajika lakini pia zinauwezo wa kutoa majibu ya papo kwa papo kwa njia ya simu ya mkononi.
Katika hatua nyingine Hospitali ya Wilaya ya Songwe kupitia jengo la dharura lenye vifaa vya kisasa lililoanza kutoa huduma toka Oktoba, 2023 limeweza kuhudumia wagonjwa 890 wa dharura hadi sasa.
