VITUO VYA DHARURA 34 VYAJENGWA
MWANZA
Kwa kipindi cha Miaka miwili 2022-2024 Serikali imejenga Vituo vipya 34 vya kutolea huduma za dharura za upasuaji hususani kwa wajawazito na kuviwekea vifaa tiba katika Mikoa ya kanda ya Ziwa ili kuendeleza adhma ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na Watoto wachanga Nchini.
Kutokana na ongezeko la vituo hivyo vya dharura imefanya kanda ya ziwa kuwa na jumla ya vituo 149 kutoka idadi ya vituo 115 vya hapo awali.
Aidha Serikali imepeleka vifaa tiba katika vituo hivyo na inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wakiwemo madaktari, wauguzi na tiba saidizi ili kuendana na mahitaji katika vituo vya kutolea huduma za afya
Vilevile idadi ya kinamama wanaojifungua katika vituo vya kutolea huduma imeongezeka kutoka 572,802 kwa mwaka 2020, hadi 692,037 kwa mwaka 2023, hii ni kutokana na kazi nzuri zinazofanywa na serikali chini serikali ya awamu ya sita.