TSH BIL 21.1 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI
DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 21.1 kwa ajili ya kununua vifaa tiba vitakavyowezesha kuboresha huduma za uzazi kwa akina mama wakiwemo wenye ulemavu katika Mwaka wa fedha 2024/2025. ( Hii ni kwa mujibu wa wizara ya afya Bungeni jijini Dodoma Septemba 4).
Pamoja na kutenga kiasi hicho cha fedha, hadi sasa Hospitali zote za Rufaa za Mikoa 28, Hospitali Sita za Kanda ambazo ni CCBRT, Mtwara, Chato, Bugando, KCMC na META Mbeya zina vyumba vya kujifungulia ikiwemo wanawake wenye ulemavu.
ZINGATIA:- Hospitali zote 184 za Halmashauri zina vyumba vya kujifungulia wakiwemo wanawake wenye ulemavu na hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.