WALIMU WARAHISHIWA UTENDAJI KAZI

 

WALIMU WARAHISHIWA UTENDAJI KAZI

WALIMU WARAHISHIWA UTENDAJI KAZI

TANZANIA
Serikali kwa kutambua umuhimu wa mazingira bora na rafiki ya kufanyia kazi kwa walimu nchini, imenunua na kusambaza vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya vituo vya walimu 501.
Vifaa hivyo ni kompyuta za mezani 1,573, kompyuta mpakato 400, televisheni janja (inch 65) 200, UPS 760, projekta 560, printa 360, mashine za kurudufu 360, zoom camera 200, na digital camera 200. 
Pia, kompyuta mpakato 159 zimenunuliwa na kusambazwa katika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Walimu za wilaya 139 na Makao Makuu ya Tume.
Aidha, walimu 400 na maafisa TEHAMA wa halmashauri 184 wamejengewa uwezo kuhusu usimikaji, matengenezo, na utoaji wa usaidizi wa kitaalamu kwa walimu kuhusu matumizi ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi wa matumizi ya teknolojia hii katika kufundishia na kujifunzia.