MIRADI 9,678 YASAJILIWA
DAR ES SALAAM
Serikali ndani ya mwaka mmoja, imefanikiwa kusajili miradi 9,678 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 8,658 (shilingi 23,636,340,000) ikilinganishwa na miradi miradi 8,401 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 5,558.47 (shilingi 15,173,341,283.1) iliyosajiliwa mwaka 2022.
Ongezeko la miradi hiyo iliyosajiliwa imeweza kuzalisha ajira za moja kwa moja 195,803 ikilinganishwa na ajira 76,841 zilizozalishwa mwaka 2022.
Aidha Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kufanya mageuzi ya uendeshaji na usimamizi wa Taasisi na Mashirika ya Umma ili kuhakikisha kwamba yanaendeshwa kwa ufanisi na tija katika kuwahudumia wananchi.
KUMBUKA: Tarehe 28 Agosti 2024 Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali alisema kwamba hivi sasa, Serikali imeridhia mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya Uwekezaji wa Umma itakayoimarisha na kuweka masharti bora ya usimamizi wa uwekezaji katika Mashirika ya Umma pamoja na kuwa na vyanzo vya uhakika vya fedha kwa ajili ya uwekezaji.