DKT SAMIA KUFUNGA TAMASHA LA UTAMADUNI MKOANI RUVUMA

 

DKT SAMIA KUFUNGA TAMASHA LA UTAMADUNI  MKOANI RUVUMA

DKT SAMIA KUFUNGA TAMASHA LA UTAMADUNI  MKOANI RUVUMA

RUVUMA
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga tamasha la tatu la utamaduni kitaifa litakalofanyika katika manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma kuanzia tarehe 20 hadi 23 septemba 2024.
Madhumuni ya tamasha hili ni pamoja na kuenzi na kulinda utamaduni, kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia ukuzaji wa sekta za ubunifu na utamaduni, kutoa jukwaa la kuonesha utamaduni kama msukumo madhubuti wa utangamano wa kitaifa kwa kuwaleta/kuwaunganisha pamoja wadau na viongozi wa sekta, kuendeleza na kuenzi urithi wa utamaduni wetu, kutoa fursa ya majadiliano ya kitaaluma baina ya wananchi wa kila mkoa, kutumia utamaduni na ubunifu kama nyenzo ya kuenzi na kukuza utambulisho wa Taifa na kutangaza fursa na rasilimali za kipekee ilizonazo nchi yetu.