VITUO VYA AFYA YA MSINGI KUFUNGWA MFUMO WA GoTHoMIS

 

VITUO VYA AFYA YA MSINGI KUFUNGWA MFUMO WA GoTHoMIS

VITUO VYA AFYA YA MSINGI KUFUNGWA MFUMO WA GoTHoMIS

DODOMA
Serikali inaendelea kuhakikisha vituo vya  kutolea huduma za Afya ya msingi nchini vinaendelea  kufungwa mfumo wa kielektroniki wa kudhibiti na kufuatilia taarifa za mteja (GoTHoMIS).
Mkoa wa Dodoma pekee jumla ya Vituo 235 vya kutolea huduma za afya vinatarajiwa kunufaika na vifaa  hivyo vilivyotolewa na Serikali ya Korea kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) linalotekeleza mradi huo Mkoani Dodoma
Ufungwaji wa mfumo huo utasaidia kupata takwimu sahihi na kuongeza ufanisi wa kazi  hasa katika sekta ya Afya.
Aidha serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI inahakikisha vituo vyote kuanzia hospital za wilaya vituo vya Afya na zahanati sasa hivi wanatoa huduma kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wa kudhibiti na kufuatilia taarifa za mteja (GoTHoMIS).