BWAWA LA MPITIMBI KUENDELEZWA

 

BWAWA LA MPITIMBI KUENDELEZWA

BWAWA LA MPITIMBI KUENDELEZWA

RUVUMA
Serikali kupitia  shirika la IFAD  imetoa kiasi cha fedha kwa ajili ya kuendeleza Bwawa la maji la asili lililopo katika Kijiji cha Mpitimbi wilayani Songea mkoani Ruvuma ili liingizwe kwenye mpango wa ufugaji endelevu wa viumbemaji.
Jumla ya shilingi bilioni 3.1 zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo katika wilaya za Songea(ikiwemo bwawa la asili ya Mpitimbi)  na Mbinga mkoani Ruvuma na Wilaya za Ruangwa na Mtama mkoani Lindi,mradi ambao unatekelezwa kwa miaka miwili kuanzia Machi 2024 hadi Machi 2026.