VIJIJI 63 VYAFANYIWA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI CHAMWINO
DODOMA
Jumla ya vijiji 63 kati ya vijiji 73 vilivyopo kwenye wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma vimefanyiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi.
Aidha, vijiji 10 vilivyosalia viko katika mchakato wa kufanyiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi katika wilaya hiyo ya Chamwino
Lengo la serikali kupitia wizara ya ardhi ni kuhakikisha mpaka kufikia Disemba, 2024 vijiji vyote wilaya ya Chamwino viwe vimefanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi na kutatua migogoro ya mipaka ya vijiji kwa kiwango kikubwa.