TSH BIL 1.7 KUMALIZA KERO YA MAJI KATA YA KITULA , MBINGA
RUVUMA
Serikali kupitia wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,umeanza kutekeleza mradi wa maji ya bomba wa Kitula kata ya Kitula Halmashauri ya wilaya Mbinga utakaowaondolea wananchi wa kata hiyo kero ya kuamka usiku wa manane na kutembea umbali mrefu kila siku kwenda kutafuta maji na kuacha shughuli za kujipatia kipato.
Mradi wa maji Kitula unatekelezwa kwa gharama ya Sh.bilioni 1.7 na utawanufaisha wananchi 9,100 wa vijiji vinne vya Mzuzu,Kitula,Mahilo na Lisau na utekelezaji wake umefikia zaidi ya 85%.
Hadi sasa kazi zinazofanyika katika mradi huo ni ujenzi wa matenki matatu moja la lita 150,000 la pili la ujazo wa lita 100,000 la tatu lina uwezo wa kuhifadhi lita 75,000 na kulaza mabomba urefu kilometa 54.