TSH BIL 3.6 ZAJENGA JENGO LA UTAWALA NA VIPIMO JKCI

 

TSH BIL 3.6  ZAJENGA  JENGO LA UTAWALA NA VIPIMO JKCI

TSH BIL 3.6  ZAJENGA  JENGO LA UTAWALA NA VIPIMO JKCI

DAR ES SALAAM
Kutokana na ongezeko la mahitaji ya huduma za matibabu ya moyo nchini,serikali ya awamu ya sita  imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 3.6 kwa lengo la kujenga jengo la utawala na vipimo ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
 Jengo hilo linalotarajiwa kumalizika  disemba mwaka huu (2024) linatarajiwa kutoa huduma za vipimo kwa wagonjwa wa moyo na magonjwa yasiyoambukiza zaidi ya 200 kwa siku hivyo kupunguza muda wa kusubiri huduma za vipimo na matibabu.
Aidha Mitambo itakayowekwa katika jengo hili l itakuwa mikubwa na ambayo inachukua muda mfupi kutoa huduma za vipimo na majibu, tunatarajia ndani ya masaa mawili mgonjwa anaweza kuwa ameshafanyiwa vipimo, kupatiwa majibu yake na kumuona daktari.
Pia jengo hilo la utawala na vipimo litatoa huduma za maabara, huduma za vipimo vya ECHO na ECG, eneo maalum kwa ajili ya wagonjwa wanaotoka nje ya nchi pamoja na vyumba vya madaktari kwa ajili ya kuwaona wagojwa ili kuwapunguzia mzunguko.