VIJANA 10,702 WAPATA MAFUNZO YA UJUZI

 

VIJANA 10,702 WAPATA MAFUNZO YA UJUZI

VIJANA 10,702 WAPATA MAFUNZO YA UJUZI

TANZANIA
Serikali imeendelea kuhakikisha inawezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi wa kuajiriwa na kujiajiri ambapo kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi, Serikali imetoa fursa za mafunzo ya ujuzi kwa vijana 10,702 katika fani mbalimbali kupitia mafunzo ya ufundi stadi kwa njia ya uanagenzi, mafunzo ya ufugaji wa samaki na viumbe maji na mafunzo ya kukuza ujuzi kwa waajiriwa wa Sekta ndogo ya Hoteli na Ukarimu. 
Aidha Serikali imewaunganisha wahitimu 2,448 na mafunzo ya utarajali na mafunzo ya kushindania fursa za ajira kwa wahitimu 7,598.