MWAKA 2023/24 FURSA ZA AJIRA 470,257 ZILIZALISHWA
TANZANIA
Katika mwaka 2023/2024, jumla ya fursa za ajira 470,257 zilizalishwa. Kati ya hizo, ajira 248,215 zilizalishwa kupitia Serikali na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ajira 222,042 kupitia sekta binafsi.
KUMBUKA:- Serikali imeendelea kuratibu masuala ya uzalishaji wa fursa za ajira nchini kupitia utekelezaji wa miradi ya kielelezo, kujenga mazingira wezeshi kwa wawekezaji na kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na sekta binafsi.