TSHS BIL 2.55 KWENYE ALAMA ZA USALAMA BARABARANI

TSHS BIL 2.55  KWENYE ALAMA ZA USALAMA BARABARANI

TSHS BIL 2.55  KWENYE ALAMA ZA USALAMA BARABARANI

DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi ( Wakala ya Barabara -TANROADS) imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 2.55 kwa ajili ya uwekaji wa alama na michoro ya usalama barabarani kwenye Barabara Kuu na zile za Mikoa.
Kwa sasa Tanzania ina jumla ya alama 183 zinazotumiwa kwa ajili ya usalama barabarani na alama 180 kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ambazo zinazotumika na nchi za Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Wanachama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).