BARABARA MANGAMBA-MSIMBATI KUJENGWA
MTWARA
Serikali imekamilisha kusanifu na inajiandaa kuanza ujenzi wa barabara ya Mang’amba – Msimbati (Km 35) na Madimba – Kilambo (Km 16) Zilizopo Mkoani Mtwara. Barabara hizo zitajengwa kwa kiwango cha lami hatua itakayosaidia kuchochea zaidi kasi ya maendeleo na uchumi.