TSH BIL 840 KUPONYA ATHARI ZA ELNINO NA KIMBUNGA HIDAYA
TANZANIA
Serikali tayari imeelekeza kiasi cha Shilingi Bilioni 840 (Dola za Marekani Milioni 325) katika ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja na makalvati yaliyoharibiwa na mvua kubwa za El-Nino na Kimbunga Hidaya ambapo maandalizi ya utekelezaji huo yanaendelea.
KUMBUKA:- mvua za El-Nino zilizonyesha katika kipindi cha mwezi Septemba 2023 hadi Aprili 2024 na kuathiri mawasiliano ya barabara na madaraja, Serikali ilitoa kiasi cha Shilingi Bilioni 72.1 kufanya matengenezo ya dharura katika maeneo yaliyokatika mawasiliano.