TSH BIL 70 KUJENGA BANDARI YA KISASA YA MBAMBA BAY
RUVUMA
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeanza kutekeleza ujenzi wa bandari mpya ya kisasa ya Mbambabay, ziwa Nyasa wilayani Nyasa mkoani Ruvuma kwa gharama ya Zaidi ya shilingi bilioni 70 lengo likiwa ni kuimarisha ushoroba wa maendeleo ya Mtwara ambayo ni njia fupi na rahisi kuhudumia mizigo ya Malawi kutokea bandari ya Mtwara.