TANZANIA NA KOREA KUSHIRIKIANA MIRADI YA BARABARA

 

TANZANIA NA KOREA KUSHIRIKIANA MIRADI YA BARABARA

TANZANIA NA KOREA KUSHIRIKIANA MIRADI YA BARABARA

DAR ES SALAAM
Serikali za Tanzania na Korea Kusini zinatarajia kushirikiana kufanya upembuzi yakinifu wa Mpango wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara za haraka (Express ways) utakaogharimu zaidi ya dola milioni 5 za Marekani (Takribani shilingi 13,622,850,000) ambazo ni msaada kutoka Korea.
Hatua hiyo imebainishwa katika mazungumzo baina ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida Mbaga na ujumbe wa wataalamu kutoka Korea uliyoambatana na Bw. Manshik Shin, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Korea nchini (KOICA).
Majadilino ya pande hizo mbili yamehusu adhima ya awali ya nchi ya Korea kuridhia kufanya upembuzi yakinifu wa mpango huo utakaokwenda sambamba na kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani kwenye eneo la utekelezaji wa miradi ya aina hiyo kwa kuwa nchi hiyo inauzoefu mkubwa wa kutekeleza miradi ya aina hiyo.