TSH BIL 226.05 KWENYE MIRADI YA MAENDELEO
TANZANIA
Katika mwaka 2023/24 shilingi bilioni 226.05 za mapato ya ndani zimetolewa kwa ajili ya kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi kinachoishia mwezi Machi 2024.
Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 50.62 zimetumika kwenye Sekta ya Elimu, shilingi bilioni 39.77 zimetumika kwenye Sekta ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii, shilingi bilioni 61.06 zimetumika kwenye Sekta ya Utawala.
Aidha, shilingi bilioni 18.92 zimetumika kwenye Sekta ya Barabara na Usafirishaji, shilingi bilioni 15.84 zimetumika kwenye Sekta ya Biashara na Uwekezaji, shilingi bilioni 13.73 zimetumika kwenye Sekta ya Ardhi na Mipango miji, shilingi bilioni 9.69 zimetumika kwenye Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, shilingi milioni 321.47 zimetumika kwenye Sekta ya Maji, na shilingi bilioni 16.06 zimetumika kwenye Sekta nyingine.