MIRADI 14 YA KIMKAKATI YAPOKEA FEDHA
TANZANIA
Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati katika mamlaka za serikali za mitaa, ambapo miradi 14 imepokea fedha.
Kati ya miradi hiyo miradi mitano (5) imekamilika ambayo ni ujenzi wa Soko la Kisasa la Kibada katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Soko la Kisasa katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Ujenzi wa Kiwanda cha Chaki katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, ujenzi wa Kituo cha Kuegesha Magari Makubwa – Nyakanazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo na upanuzi wa Kituo cha Mabasi cha Nyegezi katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Aidha, miradi tisa (9) inaendelea na utekelezaji katika hatua mbalimbali na baadhi ya miradi hiyo imeanza kutoa huduma wakati shughuli za ukamilishaji zikiendelea.