TSH BIL 1.27 ZAWANUFAISHA VIJANA

 

TSH BIL 1.27  ZAWANUFAISHA VIJANA

TSH BIL 1.27  ZAWANUFAISHA VIJANA

TANZANIA
Katika kipindi cha mwaka 2023/2024 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jumla ya mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.27 ilitolewa kwa miradi 56 ya vijana, elimu ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara kwa vijana 2,800. 
Aidha, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha uhuishaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2007 ambayo itawezesha masuala ya vijana kuratibiwa na kutekelezwa na wadau mbalimbali kwa lengo la kuinua ustawi wa vijana nchini.
ZINGATIA:- Serikali imeendelea na jitihada za uwezeshaji na uendelezaji vijana kiuchumi ili kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, kujipatia ajira na kujikwamua kiuchumi