TPA YATWAA ‘TUZO YA BANDARI BORA’ AFRIKA MASHARIKI
MWANZA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeshinda tuzo ya juu katika Maonesho ya 19 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza na kuzishinda taasisi nyingine zaidi ya 200 za kambi hiyo.
Tuzo hiyo ni matokeo ya maboresho makubwa ya huduma katika vituo vyake ambayo yamewezeshwa na uwekezaji mkubwa katika miaka ya hivi karibuni.
Pamoja na utolewaji wa tuzo hizo hafla hiyo pia imeongeza fursa za biashara na kuwezesha nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuchangamkia matarajio ya soko katika jumuiya nyingine za kikanda, ikiwa ni pamoja na Maendeleo ya Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC).