TANZANIA YAONGOZA USALAMA WA MTANDAO DUNIANI

 

TANZANIA YAONGOZA USALAMA WA MTANDAO DUNIANI

TANZANIA YAONGOZA USALAMA WA MTANDAO DUNIANI

TANZANIA
Tanzania imeorodheshwa ya kwanza Afrika Mashariki, Kusini na Kati  kuwa na usalama mtandaoni, kwa mujibu wa Ripoti mpya ya Global Cybersecurity Index (GCI) 2024 iliyotolewa hivi karibuni.
Katika viwango vya hivi karibuni vya GCI, Tanzania imepata hadhi ya Daraja la 1 katika kitengo cha Mwigizo wa Kuigwa, na kuiweka pamoja na viongozi wa kimataifa kama vile Marekani, Uingereza na Jamhuri ya Korea.
Kiwango hiki cha juu kimetengwa kwa ajili ya nchi ambazo zinaonesha kujitolea kwa mfano katika nguzo zote tano za usalama wa mtandao ambazo ni  Kisheria, Kiufundi, Kishirika, Ukuzaji wa Uwezo na Ushirikiano
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inasema mafanikio ya Tanzania yametokana na maandalizi ya kina yaliyofanyika kati ya 2023 na 2024 Kama kitovu cha Tanzania ndani ya ITU, TCRA ilichukua jukumu muhimu katika kuandika juhudi na ahadi za nchi kuhusu usalama wa mtandao.