RUVUMA WAPOKEA TSH BIL 8.25 KUBORESHA UTAWALA
RUVUMA
Serikali ya awamu ya sita imepeleka kiasi cha shilingi bilioni 8.25 kwa mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya kujenga majengo mbalimbali ya utawala, nyumba za wakurugenzi na nyumba za wakuu wa idara.
Katika fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 3.55 kimetumika kujenga jengo la ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga, ofisi ambayo imezinduliwa leo septemba 25 na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika mkoa wa Ruvuma ambapo leo ni siku ya tatu kati ya sita atakazozitumika kwa ajili ya kuzindua, kuweka mawe ya msingi, kusalimiana na wananchi pamoja kufanya mikutano ya hadhara katika Mkoa huo.
