SHULE ZA MIKOA MINNE KUNUFAIKA NA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
DODOMA
Shule za Mikoa minne ya Dar es Salaam, Kigoma, Tabora na Dodoma zinatarajia kunufaika na mradi wa nishati safi ya kupikia shuleni ambao utasaidia katika kupunguza matumzi ya kuni na mkaa yanayotokana na ukataji wa miti.Hii ni kupitia kikao kazi kilicholenga kuanzisha mradi wa matumizi ya nisharti safi ya kupikia shuleni kilichoongozwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme jijini Dodoma.
Mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Sustainable Energy for All (SEforALL).
Aidha, katika mradi huo WFP Tanzania ikishirikiana na Kituo cha Kitaifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) inatarajia kufanya uwekezaji wa nishati safi ya kupikia katika shule hizo na baadhi ya kaya nchini.
ZINGATIA:- Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na washirika wa maendeleo hususan katika jitihada zinazochagiza ajenda ya kitaifa ya nishati safi ya kupikia inayoongozwa na kinara namba moja Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.