BARABARA MNIVATA-NEWALA-MASASI INAJENGWA

 

BARABARA MNIVATA-NEWALA-MASASI INAJENGWA

BARABARA MNIVATA-NEWALA-MASASI INAJENGWA

MTWARA
Wakandarasi China Wu Yi na Ms China Communication wapo eneo la kazi kwa ajili ya kujenga barabara ya Mnivata- Newala – Masasi (Km 160) kwa kiwango cha lami.
 Ujenzi huu umegawanywa katika sehemu mbili, Mnivata- Mitesa (Km 100) ambayo inajengwa na Mkandarasi China Wu Yi na Mitesa – Masasi (Km 60) inayojengwa na Mkandarasi Ms China Communication lengo likiwa kuharakisha ujenzi huu ili kuwawezesha wananchi wa Mtwara kujiongezea kasi kwenye gurudumu la kukuza uchumi.
KUMBUKA:- Septemba 2023 Mhe.Rais Dkt Samia akiwa kwenye ziara mkoani Mtwara aliahidi kuanza kwa ujenzi wa barabara  hii na muda mfupi baada ya ziara yake,SASA KAZI INAENDELEA.