SERIKALI KUJENGA KITUO CHA KUREJELEZA TAKA ZA PLASTIKI
DODOMA
Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imesema imejipanga kujenga kituo cha kurejeleza taka za plastiki pamoja na kuhifadhi na kuchambua taka ngumu kwa ajili ya kutumika kama malighafi ya viwanda.
Kituo hicho kitakachojengwa katika Jiji la Dodoma kitasaidia ukusanyaji wa taka kutoka dampo kwa ajili ya kuchakatwa hatua itakayosaidia kulinda mazingira.
KUMBUKA:- mwaka 2021 Ofisi ya Makamu wa Rais iliandaa Mwongozo wa Udhibiti wa Taka Ngumu kuhamsisha taasisi na jamii namna ya kupunguza uzalishaji wa takaambao ulikua na dhana tatau Punguza (Reduce), kutumiwa tena (Reuse) na Rejeleza (Recycle).
Pia Mwongozo huo umeelekeza kila Halmashauri iwe na kituo cha kukusanya taka ili zirejelezwe.