DARAJA LA JPM BADO MITA 2 KUUNGANISHWA

 

DARAJA LA JPM BADO MITA 2 KUUNGANISHWA

DARAJA LA JPM BADO MITA 2 KUUNGANISHWA

MWANZA
Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye urefu wa Kilometa tatu linalojengwa kuunganisha barabara kuu ya Usagara - Sengerema - Geita katika Ziwa Victoria zimebaki sehemu ya Mita mbili  tu ili daraja lote liweze kuunganishwa.
Aidha Serikali inaendelea kuhakikisha Mkandarasi analipwa malipo yake ambapo hivi karibuni amepokea shilingi Bilioni 18 ambazo zitamuwezesha kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ifikapo mwezi Disemba 2024.
Hadi hivi sasa ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 90.5 na kazi zinaendelea kufanyika usiku na mchana ambapo matarajio hadi kufikia mwanzoni mwa Mwezi Oktoba 2024, daraja hilo litakuwa limeunganishwa.