JE UNAFAHAMU KWAMBA ¾ YA WILAYA YA NAMTUMBO NI HIFADHI
RUVUMA
Utafiti umebaini kuwa robo tatu ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ni hifadhi ikiwemo eneo la Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na ushoroba unaounganisha Selous na Niassa unaoanzia mkoani Ruvuma hadi nchini Msumbiji.
Kuna hifadhi tatu za jamii ndani ya Wilaya ya Namtumbo ambazo ni Mbarang’andu, Kisungule na Kimbanda
Wilaya ya Namtumbo inahusika katika mradi mkubwa wa umeme wa bwawa la Nyerere katika Mto Rufiji unaoendelea kutekelezwa na serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mto Luegu unaonzia Wilaya ya Namtumbo unachangia 19% ya maji katika Mto Rufiji hivyo Mkoa wa Ruvuma unahusika moja kwa moja na uendelevu wa mradi wa bwawa la Nyerere katika Mto Rufiji ambao umekusudia kuondoa mgawo wa umeme nchini.
Utalii wa uwindaji unaofanyika katika Jumuiya ya Hifadhi ya wanyamapori ya Mbarang'andu wilayani Namtumbo imekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka nchi za Ulaya na Marekani ambao wanatembelea jumuiya hiyo yenye vijiji saba na kufanya aina hiyo ya utalii ambayo inahusisha moja kwa moja matumizi ya wanyamapori.
Jumuiya hiyo inahusisha vijiji saba ambavyo ni Mchomolo, Kitanda, Likuyuseka Maganga, Kilmasela, Nambecha, Songambele na Mtelemwahi.
#BIMKUBWAKAZINIRUVUMA