DKT SAMIA AKAGUA KIWANJA CHA NDEGE SONGEA
RUVUMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan leo septemba 23, 2024 amekagua ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Songea kilichopo Mkoani Ruvuma ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku 6 mkoani humo,Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 40.873 kwa ajili ya kufanya maboresho makubwa ya kiwanja hicho.