DKT SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MTYANGIMBOLE
RUVUMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan leo septemba 24 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji wa Mtyangimbole uliopo wilayani Songea Mkoani Ruvuma.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi 30 ya maji inayoendelea kutekelezwa katika mkoa wa Ruvuma ambayo inagahrimu kiasi cha shilingi bilioni 58
Mradi wa maji wa Mtyangimbole utahudumia wananchi wapatao elfu 14 kutoka katika vijiji vitatu vya Luhimba lukalangilo na Mtyangimbole vinavyopatikana katika jimbo la madaba Mkoani Ruvuma
Vilevile mwaka 2023/2024 mkoa wa Ruvuma umetekeleza miradi 24 amabyo tayari imekamilika na imegharimu takribani shilingi bilionin 25.
