UWEKEZAJI WA BANDARI YA TANGA WALETA MATUNDA
TANGA
Uwekezaji uliofanyika katika Bandari ya Tanga umeanza kuzaa matunda huku meli kubwa kutoka nje ya nchi zikitia nanga katika bandari hiyo.
Hivi karibuni, Kampuni ya Seafront Shipping Services Limited (SSS) ilifanikiwa kuzindua meli ya kwanza ya mizigo ya jumla, ikisafirisha takribani tani 14,000 za bidhaa kutoka China hadi Bandari ya Tanga.
Mizigo hiyo inapelekwa nchi mbalimbali, zikiwemo Zambia, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malawi, Rwanda na nyinginezo.
Pia Meli ya ‘MV Annegrit’ yenye urefu wa mita 200 iliwasili wiki jana baada ya safari ya siku 21 kutoka Guangdong, na kuashiria hatua muhimu kwa bandari hiyo.
Maboresho katika bandari ya Tanga yamefanikisha ongezeko la meli katika Bandari hiyo kutoka meli 118 mwaka 2019/20 hadi 307 mwaka 2022/23.
ZINGATIA:- Serikali imeboresha Bandari ya Tanga ili kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam pia imekamilisha uboreshaji wa njia ya reli inayounganisha Njia ya Kati hadi Bandari ya Tanga kupitia Stesheni ya Ruvu.