TSH BIL 843 ZAJENGA HOSPITALI 129 NCHINI
TANZANIA
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa Sh.Bilioni 843 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya 129 nchini.
Fedha hizo zimetumika kuboresha zaidi upatikanaji wa huduma za Afya na hadi sasa Wilaya zote nchini zina Hospitali za Wilaya.
Pia zaidi ya Sh. Bilioni 283 zimetumika kununua vifaa tiba na kati ya fedha hizo sh.Bilioni 4.1 zimetumika kusomesha wataalam wa Afya 570.