DKT SAMIA ASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

 

DKT SAMIA ASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

DKT SAMIA ASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

MOROGORO
Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kote nchini kuweka kipaumbele katika uhifadhi wa mazingira, ili kuzuia upotevu wa viumbe hai na kulinda maliasili.
Katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya CCM-Ifakara mkoani Morogoro Agosti 5, Mkuu huyo wa nchi pia amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji ikiwemo mito ambayo ni muhimu kwa maisha ya binadamu na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akihutubia umati wa watu kama sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo, Rais Samia ameeleza 
"Unapofuga katika maeneo oevu na chemchemi, unaharibu vyanzo vya asili vya maji,nawaomba tuhifadhi mazingira. Ni lazima tuhifadhi maliasili zetu kwa matumizi ya sasa na yajayo,” amesema Rais Samia
Rais Samia amehusisha sehemu ya uharibifu wa ikolojia ya Morogoro na shughuli za kiuchumi katika maeneo oevu, ambayo ni muhimu kwa kuendeleza mito na vijito. Hii imedhoofisha uwezo wa Bonde la Mto Kilombero kukusanya maji ya kutosha.
Aidha Rais Samia pia amewaagiza viongozi wa mitaa wakiwemo Madiwani wa Kata na Wabunge kuepuka kuanzisha vijiji vipya kwenye maeneo ya hifadhi kwa maslahi ya kisiasa.