TSH MIL 636 ZAJENGA KITUO CHA AFYA KINYEREZI
Kiasi cha shilingi milioni 636 zimekamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Cha Kinyerezi kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam ambacho kina Jumla ya Majengo Matatu ya Kisasa kwa ajili ya kutoa huduma za Afya.
Majengo hayo ni Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD), Jengo la Wazazi na Jengo la Upasuaji
Sasa Wakazi wa Maeneo Ya Kinyerezi na Maeneo Jirani hawapati tena usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kupata huduma bora za Afya kwakuwa zimeshasogezwa karibu na Wananchi.