TSH BIL 9.68 ZAJENGA SOKO TARIME
Kiasi cha shilingi bilioni 9.68 kimetumika kukamilisha ujenzi wa soko la kisasa katika Halmashauri ya wilaya Tarime mkoani Mara.
Mradi huo wa soko una maduka 325, vizimba 160, mabucha matatu, migahawa miwili, supermarket moja na Benki mbili, ujenzi ulianza 19/1/2022 na kukamilika 2024.