TSH BIL 44+ KUFIKISHA MAJI USHETU

 

TSH BIL 44+ KUFIKISHA MAJI USHETU

TSH BIL 44+ KUFIKISHA MAJI USHETU

SHINYANGA
Mkataba wa shilingi 44,271,886,678.17 wa kutoa maji ya ziwa Victoria Kahama hadi Ushetu mkoani Shinyanga umesainiwa ambao utaanza utekelezaji hivi karibuni na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 24.
Utekelezaji wake utahusisha ujenzi wa matanki matatu (3) yenye ujazo wa lita 500,000, 300,000 na 100,000 katika maeneo tofauti ndani ya Kata ya Ulowa Pamoja na ujenzi wa bomba kuu lenye kipenyo cha kuanzia milimita 350 hadi milimita 100 lenye urefu wa kilometa 76 kutoka Manispaa ya Kahama kwenda Ulowa hadi kwenye matanki. 
Pia ujenzi wa mfumo wa kutibu maji na ujenzi wa vituo 35 vya kuchotea maji na ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji wenye bomba aina HDPE zenye urefu wa KM 74 pamoja na vituo vya kuchotea maji 35.
Aidha jumla ya wananchi wapatao 189,836 wa Kata za Igunda, Kisuke, Kinamapula, Nyamilangano, Mapamba, Uyogo, Bukomela, Ushetu na Ulowa watanufaika na mradi huu.